Jumapili, 24 Septemba 2017

Viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini watupiana vitisho vipya


Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionViongozi wa Marekani na Korea Kaskazini watupiana vitisho vipya

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa vitisho vipya kwa Korea Kaskazini kuhusu hutuba kali ya waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Korea Kaskazini kweye Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi.
Ri Yong-ho alimtaja Bw Trump kama mtu aliye na matatizo ya akili aliye katika mikakati ya kujitia kitanzi.
Rais wa Marekani alijibu kwa kusema kuwa Bw Ri na kiongozi wa Korta Kaskazini Kim Jong-un hawatakuwepo kwa muda mrefu, ikiwa wataendelea na matamshi yao.
Majabizano hayo mapya yanatolewa wakati ndege za jeshi la Marekani zinaruka karibu na Korea Kaskazini.
Makao makuu ya ulinzi nchini Marekani yanasema kuwa lengo lilikuwa ni kuonyesha ubabe wa kijeshi wa Marekani uliopo kukabiliana na tisho lolote.

US Air Force B-1B LancerHaki miliki ya pichaUS PACIFIC COMMAND
Image captionMajabizano hayo mapya yanatolewa wakati ndege za jeshi la Marekani zinaruka karibu na Korea Kaskazini.

Pentagon ilisema kuwa eneo hilo ndilo eneo mbali zaidi kati ya mpaka wenye ulinzi mkali kati ya Korea mbili ambapo ndege za Marekani zimepitia katika karne ya 21.
Misuko suko imeongezeka hivi majuzi kufuatia mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
Matamshi ya Bw Yong-ho kwa Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi yaliiga yale yaliyotolewa na Trump siku ya Jumanne kwa UN, wakati alimuita Kim Jong-un kuwa mtu wa makombora aliye kwenye mikakati ya kujitia kitanzi.BBC SWAHILI

Ndege za kijeshi za Marekani zapaa karibu na Korea Kaskazini kuonyesha ubabe

Ndege za kijeshi za Marekani zimepaa karibu na pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini katika kuonyesha ubabe wa kivita, idara ya ulinzi nchini Marekani pentagon imesema.
''Hatua hiyo ni kuonyesha kuwa rais Trump ana njia tofauti za kijeshi kushinda vitisho vyovyote'' , msemaji Dana White alisema.

Marekani na Korea Kaskazini zimerushiana cheche za maneneo katika kipindi cha hivi majuzi.

Katika Umoja wa mataifa siku ya Jumanne, bwana Trump alisema kuwa ataiangamiza Korea Kaskazini iwapo Marekani italazimika kujitetea na washirika wake.

''Hili ni eneo ambalo jeshi lolote halifai kupitia na ni ndege za kijeshi za Marekani ambazo zimeweza kulifikia katika karne ya 21, licha ya tabia mbaya ya Korea Kaskazini'', alisema Bi White.

Tangazo hili lilijiri muda mfupi kabla ya waziri wa kigeni wa Korea Kaskazini kutoa hotuba yake katika umoja wa mataifa.

Mapema siku ya Jumamosi , tetemeko lenye ukubwa wa 3.4 katika vipimo vya Ritcher lilisikika karibu na kituo cha kujaribia makombora cha Korea Kaskazini na kuzua hofu kwamba taifa hilo huenda lilitekeleza jaribio jingine la kombora lake.

Lakini wataalam wamesema kuwa lilikuwa tetemeko la ardhi.

Mke wa Tundu Lissu, Dreva Wake Wafunguka kwa Mara ya Kwanza

Kwa mara ya kwanza, Alicia Magabe ambaye ni mke wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia tukio la mumewe kushambuliwa kwa risasi na kudokeza kwamba haliwezi kuwa limetokana na sababu nyingine isipokuwa kazi ambazo amekuwa akizifanya.

Pia amezungumzia kuhusu afya yake na kueleza kuwa bado siyo nzuri na kuwaomba Watanzania waendelee kumuombea.
Mbali ya Alicia ambaye pia ni mwanasheria, dereva wa Lissu naye amezungumza akisema ameathiriwa kwa kiasi kikubwa na tukio hilo huku akiahidi kuripoti polisi mara baada ya kurejea nchini.

Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), amelazwa katika Hospitali ya Nairobi tangu alipopelekwa huko baada ya kupigwa risasi akiwa ndani ya gari nje ya nyumba yake mjini Dodoma mchana wa Septemba 7 akitokea bungeni.

“Watanzania wote wanajua Lissu maisha yake yote amekuwa ni mtetezi wa wanyonge na tukio hili amelipata kutokana na kazi zake hizo hivyo nawaomba tumuombee tu,” alisema.

“Ninachoweza kusema hali ya mheshimiwa Lissu sio nzuri ingawa ni tofauti na tulivyomleta hapa, hivyo naomba Watanzania kuendelea kumuombea.”

Aliwashukuru Watanzania kwa michango, na maombi yao kwa Lissu akisema hiyo inaonyesha ni jinsi gani wanathamini mchango wake kwa jamii.

Alipoulizwa kuhusu kauli ya Serikali kwamba ipo tayari kugharimia matibabu ya Lissu popote ikiwa itaombwa na familia hiyo, Alicia ambaye pia ni wakili alisema kwa sasa hana maoni.

“Katika hili no comment (sina maoni) ndio tumesikia jana amezungumza na kwa kuwa jambo hili siyo la uamuzi wa mtu mmoja, mimi sina cha kusema,” alisema.

Hata hivyo, alisema anashukuru kazi kubwa ambayo inafanywa na madaktari wa Hospitali ya Nairobi na kusema wanaridhishwa na matibabu ambayo anapatiwa kwa sasa.

Kauli  ya  Dereva wa Lissu
Mbali ya Alicia, dereva wa Lissu ambaye ndiye mtu pekee waliyekuwa wote siku ya tukio hilo, Simon Bakari naye alizungumza kwa mara ya kwanza kuhusu tukio hilo na kudokeza kwamba limevuruga na hana kumbukumbu sahihi.

Dereva huyo ambaye naye anaendelea kupatiwa matibabu ya kisaikolojia katika hospitali hiyo ya Nairobi alisisitiza, “Kwa sasa siwezi kuzungumza vizuri tukio hili kwani nadhani sina kumbukumbu vizuri.”

Alipoulizwa kuhusu wito wa polisi wa kwenda kutoa maelezo, alisema atafanya hivyo pindi atakaporejea nchini baada ya matibabu.

“Nilisikia polisi wamenitaka nikatoe maelezo lakini sijisikii vizuri na bado napata matibabu. Nitakwenda,” alisema.

Paris St-Germain wapoteza alama kwa kutoka sare na Montpelleir

Paris St-Germain ilipoteza alama katika ligi ya kwanza kwa mara ya kwanza msimu huu, bila ya kuwepo Neymar walipotoka sare ya sufuri na Montpelleir.
Neymar ambaye alitofautiana na Edinson Cavani kuhusu ni nani angepiga penalti katika mechi yao ya mwisho na Lyon, anaaminiwa kuwa na jeraha dogo la mguu.
Kylina Mbappe aliokoa mara mbili kutoka kwa Benjamin Lecomte lakini pia mchezo wa PSG haukuwa mzuri.
Kwa sasa wako pointi moja juu ya mabingwa Monaco ambao waliwapa kichapo cha mabao 4-0 Lille siku ya Ijumaa.Edinson Cavani and Kylian Mbappe

Diwani wa CHADEMA Arusha aachia ngazi mbele ya JPM

Katika hali ambayo haikutarajiwa, Diwani wa Kata ya Kimandolu Jiji la Arusha (Chadema), Mchungaji Rayson Ngowi akiongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ametangaza kumuunga mkono Rais John Magufuli na kwa kuachia nafasi yake.
Alifanya hivyo jana mbele Rais Magufuli wakati madiwani 10 wa Chadema waliojiuzulu nafasi zao kwa nyakati tofauti kwenye halmashauri tatu za Arusha na kujiunga na CCM walipoitwa wakati Rais alipokuwa akihutubia baada ya kutunuku kamisheni kwa maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Hatua hiyo inafanya jiji la Arusha linaloongozwa na Chadema kupoteza kata mbili.
Madiwani wengine waliojitambulisha mbele ya Rais Magufuli ni wale waliojiuzulu katika halmashauri za Meru na Arusha Vijijini.
Mchungaji Ngowi ndiye aliyekuwa wa kwanza kupanda jukwaani na kuanza kumwagia sifa Rais Magufuli, “Mwanzoni nilikuwa sikuelewi lakini sasa nakuelewa sana. Nataka Watanzania wote wakuunge mkono. Tunaona jitihada zako za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya asali na maziwa. Tuko pamoja na nashukuru sana kwa kunipokea.”
Mwingine aliyepanda jukwaani ni aliyekuwa Diwani wa Muriet, Credo Kifukwe ambaye alisema, “Nimeamua kumuunga mkono Magufuli kutokana na kazi nzuri alizofanya na kila mwenye akili timamu anaona. Huko tulikokuwa ilikuwa mambo ya pingapinga hawataki kuona mazuri yanayoendelea, nimeamua kurudi CCM hapa kazi tu.”
Baadaye Rais Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM alisema, “Hawa wananchi wanataka maendeleo kuliko majina ya vyama na maendeleo hayajali wewe ni CCM , Chadema au CUF.”
Hata hivyo, alionyeshwa kushangazwa na madiwani hao kuacha haki zao zikiwamo masilahi mengine na kuamua kujizulu nafasi zao na kuwakaribisha CCM.
Pia, aliutaka uongozi wa CCM kuwapitisha madiwani hao kuwania tena nafasi hizo ili wakashindane na vyama vingine.

Watu sita wajeruhiwa kwenye shambulizi la tindi kali London

Watu 6 wamejeruhiwa huko Stratford mashariki mwa London kwenye kile kinachotajwa kuwa shambulizi la tindi kali.
Polisi waliitwa kwenda huko Stratford kufuatia makabiliano kati ya makundi mawili ya wanaume ambapo kitu kilirushwa.
Watoa huduma za dharura waliwatibu wanaume sita katika eneo hilo na watatu kati yao wakapelekwa hospitalini.
Kijana wa kiume wa umri wa miaka 15 amekamatwa kwa kushukiwa kusababisha majeraha mabaya ya mwili.Police speaking to people outside Stratford CentreWale walioripotiwa kujehiwa waliaminiwa kuwa maeneo tofauti hali iliyozua kuwa watu walikuwa wamerushiwa tindi kali hiyo kiholela.
Hata hivyo polisi walisema kuwa wale waliojeruhiwa walikuwa walihusika na shambulizi la awali.Hakuna mtu aliyepaya majeraha ya kutishia maisha au kubadilisha maisha.Walioshuhudia wanasema kuwa majibizano yalikuwa yamezuka kati ya kundi la watu.
Mwanamume mmoja ambaye alitajwa jina kama Hossen ambaye ni meneja wa mgahawa mmoja, alisema kwa muathiriwa akikimbia kwenda kwa mgahawa kuasha kuosha tindi kali hiyo kutoka kwa uso wake.
"Alikuwa na majeraha kwenye uso na alikuwa anajaribu kuyamwagia maji," alisema Hossen.

Jumamosi, 23 Septemba 2017

Diego Costa: Singependa kuondoka Chelsea na machungu

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa anasema kuwa hakupenda kuondoka Chelsea ''kwa machungu' na kwamba amekuwa akiipenda klabu hiyo.
Klabu ya Atletico Madrid imefanya makubaliano na Chelsea ya kumrudisha mshambuliaji huyo ,28, katika klabu hiyo ya Uhispania.
Costa hajaichezea klabu hiyo msimu huu na ametumikia kipindi kirefu cha mwezi Agosti akiwa Brazil alikozaliwa.
''Sitaondoka bila kuishukuru Chelsea, ambapo nilifurahia kuwepo kuichezea timu kubwa'', alisema Costa baada ya kuwasili Madrid. ''Atletico ndio nyumbani kwangu''.
Uhamisho huo ambao utakamilishwa mnamo mwezi Januari unashirikisha makubaliano ya kibinafsi.
Atletico imesema kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 28 ambaye aliondoka klabu hiyo na kujiunga na Chelsea 2014 atafanyiwa ukaguzi wa kimatibabu siku chache zijazo.Diego Costa