Jumapili, 24 Septemba 2017

Viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini watupiana vitisho vipya


Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionViongozi wa Marekani na Korea Kaskazini watupiana vitisho vipya

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa vitisho vipya kwa Korea Kaskazini kuhusu hutuba kali ya waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Korea Kaskazini kweye Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi.
Ri Yong-ho alimtaja Bw Trump kama mtu aliye na matatizo ya akili aliye katika mikakati ya kujitia kitanzi.
Rais wa Marekani alijibu kwa kusema kuwa Bw Ri na kiongozi wa Korta Kaskazini Kim Jong-un hawatakuwepo kwa muda mrefu, ikiwa wataendelea na matamshi yao.
Majabizano hayo mapya yanatolewa wakati ndege za jeshi la Marekani zinaruka karibu na Korea Kaskazini.
Makao makuu ya ulinzi nchini Marekani yanasema kuwa lengo lilikuwa ni kuonyesha ubabe wa kijeshi wa Marekani uliopo kukabiliana na tisho lolote.

US Air Force B-1B LancerHaki miliki ya pichaUS PACIFIC COMMAND
Image captionMajabizano hayo mapya yanatolewa wakati ndege za jeshi la Marekani zinaruka karibu na Korea Kaskazini.

Pentagon ilisema kuwa eneo hilo ndilo eneo mbali zaidi kati ya mpaka wenye ulinzi mkali kati ya Korea mbili ambapo ndege za Marekani zimepitia katika karne ya 21.
Misuko suko imeongezeka hivi majuzi kufuatia mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
Matamshi ya Bw Yong-ho kwa Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi yaliiga yale yaliyotolewa na Trump siku ya Jumanne kwa UN, wakati alimuita Kim Jong-un kuwa mtu wa makombora aliye kwenye mikakati ya kujitia kitanzi.BBC SWAHILI

Ndege za kijeshi za Marekani zapaa karibu na Korea Kaskazini kuonyesha ubabe

Ndege za kijeshi za Marekani zimepaa karibu na pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini katika kuonyesha ubabe wa kivita, idara ya ulinzi nchini Marekani pentagon imesema.
''Hatua hiyo ni kuonyesha kuwa rais Trump ana njia tofauti za kijeshi kushinda vitisho vyovyote'' , msemaji Dana White alisema.

Marekani na Korea Kaskazini zimerushiana cheche za maneneo katika kipindi cha hivi majuzi.

Katika Umoja wa mataifa siku ya Jumanne, bwana Trump alisema kuwa ataiangamiza Korea Kaskazini iwapo Marekani italazimika kujitetea na washirika wake.

''Hili ni eneo ambalo jeshi lolote halifai kupitia na ni ndege za kijeshi za Marekani ambazo zimeweza kulifikia katika karne ya 21, licha ya tabia mbaya ya Korea Kaskazini'', alisema Bi White.

Tangazo hili lilijiri muda mfupi kabla ya waziri wa kigeni wa Korea Kaskazini kutoa hotuba yake katika umoja wa mataifa.

Mapema siku ya Jumamosi , tetemeko lenye ukubwa wa 3.4 katika vipimo vya Ritcher lilisikika karibu na kituo cha kujaribia makombora cha Korea Kaskazini na kuzua hofu kwamba taifa hilo huenda lilitekeleza jaribio jingine la kombora lake.

Lakini wataalam wamesema kuwa lilikuwa tetemeko la ardhi.

Mke wa Tundu Lissu, Dreva Wake Wafunguka kwa Mara ya Kwanza

Kwa mara ya kwanza, Alicia Magabe ambaye ni mke wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia tukio la mumewe kushambuliwa kwa risasi na kudokeza kwamba haliwezi kuwa limetokana na sababu nyingine isipokuwa kazi ambazo amekuwa akizifanya.

Pia amezungumzia kuhusu afya yake na kueleza kuwa bado siyo nzuri na kuwaomba Watanzania waendelee kumuombea.
Mbali ya Alicia ambaye pia ni mwanasheria, dereva wa Lissu naye amezungumza akisema ameathiriwa kwa kiasi kikubwa na tukio hilo huku akiahidi kuripoti polisi mara baada ya kurejea nchini.

Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), amelazwa katika Hospitali ya Nairobi tangu alipopelekwa huko baada ya kupigwa risasi akiwa ndani ya gari nje ya nyumba yake mjini Dodoma mchana wa Septemba 7 akitokea bungeni.

“Watanzania wote wanajua Lissu maisha yake yote amekuwa ni mtetezi wa wanyonge na tukio hili amelipata kutokana na kazi zake hizo hivyo nawaomba tumuombee tu,” alisema.

“Ninachoweza kusema hali ya mheshimiwa Lissu sio nzuri ingawa ni tofauti na tulivyomleta hapa, hivyo naomba Watanzania kuendelea kumuombea.”

Aliwashukuru Watanzania kwa michango, na maombi yao kwa Lissu akisema hiyo inaonyesha ni jinsi gani wanathamini mchango wake kwa jamii.

Alipoulizwa kuhusu kauli ya Serikali kwamba ipo tayari kugharimia matibabu ya Lissu popote ikiwa itaombwa na familia hiyo, Alicia ambaye pia ni wakili alisema kwa sasa hana maoni.

“Katika hili no comment (sina maoni) ndio tumesikia jana amezungumza na kwa kuwa jambo hili siyo la uamuzi wa mtu mmoja, mimi sina cha kusema,” alisema.

Hata hivyo, alisema anashukuru kazi kubwa ambayo inafanywa na madaktari wa Hospitali ya Nairobi na kusema wanaridhishwa na matibabu ambayo anapatiwa kwa sasa.

Kauli  ya  Dereva wa Lissu
Mbali ya Alicia, dereva wa Lissu ambaye ndiye mtu pekee waliyekuwa wote siku ya tukio hilo, Simon Bakari naye alizungumza kwa mara ya kwanza kuhusu tukio hilo na kudokeza kwamba limevuruga na hana kumbukumbu sahihi.

Dereva huyo ambaye naye anaendelea kupatiwa matibabu ya kisaikolojia katika hospitali hiyo ya Nairobi alisisitiza, “Kwa sasa siwezi kuzungumza vizuri tukio hili kwani nadhani sina kumbukumbu vizuri.”

Alipoulizwa kuhusu wito wa polisi wa kwenda kutoa maelezo, alisema atafanya hivyo pindi atakaporejea nchini baada ya matibabu.

“Nilisikia polisi wamenitaka nikatoe maelezo lakini sijisikii vizuri na bado napata matibabu. Nitakwenda,” alisema.

Paris St-Germain wapoteza alama kwa kutoka sare na Montpelleir

Paris St-Germain ilipoteza alama katika ligi ya kwanza kwa mara ya kwanza msimu huu, bila ya kuwepo Neymar walipotoka sare ya sufuri na Montpelleir.
Neymar ambaye alitofautiana na Edinson Cavani kuhusu ni nani angepiga penalti katika mechi yao ya mwisho na Lyon, anaaminiwa kuwa na jeraha dogo la mguu.
Kylina Mbappe aliokoa mara mbili kutoka kwa Benjamin Lecomte lakini pia mchezo wa PSG haukuwa mzuri.
Kwa sasa wako pointi moja juu ya mabingwa Monaco ambao waliwapa kichapo cha mabao 4-0 Lille siku ya Ijumaa.Edinson Cavani and Kylian Mbappe

Diwani wa CHADEMA Arusha aachia ngazi mbele ya JPM

Katika hali ambayo haikutarajiwa, Diwani wa Kata ya Kimandolu Jiji la Arusha (Chadema), Mchungaji Rayson Ngowi akiongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ametangaza kumuunga mkono Rais John Magufuli na kwa kuachia nafasi yake.
Alifanya hivyo jana mbele Rais Magufuli wakati madiwani 10 wa Chadema waliojiuzulu nafasi zao kwa nyakati tofauti kwenye halmashauri tatu za Arusha na kujiunga na CCM walipoitwa wakati Rais alipokuwa akihutubia baada ya kutunuku kamisheni kwa maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Hatua hiyo inafanya jiji la Arusha linaloongozwa na Chadema kupoteza kata mbili.
Madiwani wengine waliojitambulisha mbele ya Rais Magufuli ni wale waliojiuzulu katika halmashauri za Meru na Arusha Vijijini.
Mchungaji Ngowi ndiye aliyekuwa wa kwanza kupanda jukwaani na kuanza kumwagia sifa Rais Magufuli, “Mwanzoni nilikuwa sikuelewi lakini sasa nakuelewa sana. Nataka Watanzania wote wakuunge mkono. Tunaona jitihada zako za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya asali na maziwa. Tuko pamoja na nashukuru sana kwa kunipokea.”
Mwingine aliyepanda jukwaani ni aliyekuwa Diwani wa Muriet, Credo Kifukwe ambaye alisema, “Nimeamua kumuunga mkono Magufuli kutokana na kazi nzuri alizofanya na kila mwenye akili timamu anaona. Huko tulikokuwa ilikuwa mambo ya pingapinga hawataki kuona mazuri yanayoendelea, nimeamua kurudi CCM hapa kazi tu.”
Baadaye Rais Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM alisema, “Hawa wananchi wanataka maendeleo kuliko majina ya vyama na maendeleo hayajali wewe ni CCM , Chadema au CUF.”
Hata hivyo, alionyeshwa kushangazwa na madiwani hao kuacha haki zao zikiwamo masilahi mengine na kuamua kujizulu nafasi zao na kuwakaribisha CCM.
Pia, aliutaka uongozi wa CCM kuwapitisha madiwani hao kuwania tena nafasi hizo ili wakashindane na vyama vingine.

Watu sita wajeruhiwa kwenye shambulizi la tindi kali London

Watu 6 wamejeruhiwa huko Stratford mashariki mwa London kwenye kile kinachotajwa kuwa shambulizi la tindi kali.
Polisi waliitwa kwenda huko Stratford kufuatia makabiliano kati ya makundi mawili ya wanaume ambapo kitu kilirushwa.
Watoa huduma za dharura waliwatibu wanaume sita katika eneo hilo na watatu kati yao wakapelekwa hospitalini.
Kijana wa kiume wa umri wa miaka 15 amekamatwa kwa kushukiwa kusababisha majeraha mabaya ya mwili.Police speaking to people outside Stratford CentreWale walioripotiwa kujehiwa waliaminiwa kuwa maeneo tofauti hali iliyozua kuwa watu walikuwa wamerushiwa tindi kali hiyo kiholela.
Hata hivyo polisi walisema kuwa wale waliojeruhiwa walikuwa walihusika na shambulizi la awali.Hakuna mtu aliyepaya majeraha ya kutishia maisha au kubadilisha maisha.Walioshuhudia wanasema kuwa majibizano yalikuwa yamezuka kati ya kundi la watu.
Mwanamume mmoja ambaye alitajwa jina kama Hossen ambaye ni meneja wa mgahawa mmoja, alisema kwa muathiriwa akikimbia kwenda kwa mgahawa kuasha kuosha tindi kali hiyo kutoka kwa uso wake.
"Alikuwa na majeraha kwenye uso na alikuwa anajaribu kuyamwagia maji," alisema Hossen.

Jumamosi, 23 Septemba 2017

Diego Costa: Singependa kuondoka Chelsea na machungu

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa anasema kuwa hakupenda kuondoka Chelsea ''kwa machungu' na kwamba amekuwa akiipenda klabu hiyo.
Klabu ya Atletico Madrid imefanya makubaliano na Chelsea ya kumrudisha mshambuliaji huyo ,28, katika klabu hiyo ya Uhispania.
Costa hajaichezea klabu hiyo msimu huu na ametumikia kipindi kirefu cha mwezi Agosti akiwa Brazil alikozaliwa.
''Sitaondoka bila kuishukuru Chelsea, ambapo nilifurahia kuwepo kuichezea timu kubwa'', alisema Costa baada ya kuwasili Madrid. ''Atletico ndio nyumbani kwangu''.
Uhamisho huo ambao utakamilishwa mnamo mwezi Januari unashirikisha makubaliano ya kibinafsi.
Atletico imesema kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 28 ambaye aliondoka klabu hiyo na kujiunga na Chelsea 2014 atafanyiwa ukaguzi wa kimatibabu siku chache zijazo.Diego Costa

Mbowe Atoa Sababu Kwa Nini Hawajafungua Kesi Yoyote Dhidi ya Shambulio la Tundu Lissu


Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe amefunguka na kujibu hoja za kwa nini mpaka sasa CHADEMA hawajafungua kesi kutokana na shambulio Tundu Lissu  ambapo amesema ni kutokana na kuwa kipaumbele chao cha kwanza ni kuokoa maisha ya Lissu.


Mh. Mbowe ameyasema hayo wakati akizungumza jana na wanahabari ambapo amesema kuwa baada ya tukio la Lissu kutokea akili na mawazo ya Chadema yalikuwa kwenye kuokoa maisha ya Lissu na wanasubiri mambo yakiwa sawa wataangalia kufanya lolote linalowezekana kwan wakati huo.

"Kwa nini Chadema hatujafungua kesi? Kesi unafungua kwa nani? Anayechunguza ni nani? Chadema tumeshafungua kesi nyingi ya akiwepo Ben Saanane msaidizi wangu aliye[potea kusikojulikana, Kesi ya nyani unapeleka kwa Tumbili. Priority yetu sisi ni kumuokoa Lissu na siyo Kesi. Kupigania maisha yake ndicho kitu tuliona kinachofaa kufanywa na ndicho tunachofanya mpaka sasa", amesema.

"Ninaamini tu mambo yakikaa sawa vichwa vyote hivi vya Chadema vitajua kama tunaweza kufungua kesi au kitu gani kingine ambacho kinafaa kufanywa endapo tu afya ya Mh. Lissu ikishaimarika" ameongeza

Akizungumzia kwanini mpaka leo dereva wa Lissu hajarudi nchini ili kwenda kuripoti polisi kama jinsi jeshi la polisi lilivyoagiza, Mbowe amesema kwamba kijana huyo atarudishwa nchini pindi tuu wataalamu wa afya wanaomhudumia wakitoa ripoti afya yake kama iko salama na wao hawapo kwa ajili ya kumficha.

"Wiki iliopita nilisema dereva wa Mh. Lissu yupo Nairiobi kwa ajili ya matibabu ya kisaikolojia. Hatukuona kama ni busara kumtelekeza wakati alikuwepo kwenye matatizo na boss wake. Madaktari wakituthibitishia kuwa yuko timamu atarudi nchini kwani hatuko kwa ajili ya kumficha mtu. Yule kijana ni kama mtoto wa Lissu, dereva na mlinzi wake, wana miaka mingi pamoja tangu Lissu anagombea ubunge kwa mara ya kwanza" amesisitiza.

Ameongeza pia dereva atakuja kuzungumza nini kilitokea na yeye alijiokoaje naamini aliyekuwa anashambulia alikuwa hajalenga kumuacha hai mtu hata mmoja hivyo mimi siyo msemaji sana wa dereva wake Lissu lakini akipona ataelezea mwenyewe kila kitu.

DIAMOND,MOHOMBI,LUMINO LIVE PERFORMANCE

LUMINO-ROCKONOLO[REMIX]

MIMI MARS-SHUGA

MIMI MARS-DEDEE

RAYVANNY-UNAIBIWA

DESPACITO-VIOLA KARURI

SANAPEI TANDE-AMINA

Diego Costa: Singependa kuondoka Chelsea na machungu

Diego Costa
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa anasema kuwa hakupenda kuondoka Chelsea ''kwa machungu' na kwamba amekuwa akiipenda klabu hiyo.
Klabu ya Atletico Madrid imefanya makubaliano na Chelsea ya kumrudisha mshambuliaji huyo ,28, katika klabu hiyo ya Uhispania.
Costa hajaichezea klabu hiyo msimu huu na ametumikia kipindi kirefu cha mwezi Agosti akiwa Brazil alikozaliwa.
''Sitaondoka bila kuishukuru Chelsea, ambapo nilifurahia kuwepo kuichezea timu kubwa'', alisema Costa baada ya kuwasili Madrid. ''Atletico ndio nyumbani kwangu''.
Uhamisho huo ambao utakamilishwa mnamo mwezi Januari unashirikisha makubaliano ya kibinafsi.
Atletico imesema kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 28 ambaye aliondoka klabu hiyo na kujiunga na Chelsea 2014 atafanyiwa ukaguzi wa kimatibabu siku chache zijazo.

Trump na Kim Jong-Un waitana ''wenda wazimu''

Rais Kim Jong Un na mwenzake wa Donald Trump
Rais Kim Jong Un na mwenzake wa Donald Trump

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amesema kuwa matamshi ya rais wa Marekani Donald Trump aliyemtaja kuwa ''na matatizo ya kiakili'' yamempatia motisha zaidi ya kuendelea kutengeza makombora ya taifa lake.
Katika taarifa ya kibinafsi isio ya kawaida, bwana Kim amesema kuwa rais Trump ''atalipia kauli'' zake za hotuba ya baraza la Umoja wa mataifa ambapo alionya kuiangamiza Korea Kaskazini iwapo Marekani italazimika kujilinda.
Bwana Trump naye alijibu akisema kuwa ''mwenda wazimu'' hajawahi kufanyiwa atakachofanyiwa akijaribu.
Mataifa hayo mawili wamejibizana kwa kurushiana maneneo makali katika siku za hivi karibuni.
Rais Kim alimaliza taarifa yake kwa kusema kwamba atamnyamazisha kiongozi huyo ''aliye na akili punguani'' kwa vita.
China ilijibu vita hivyo vya maneno ikionya kuwa hali ni mbaya.
''Pande zote zinafaa kujikaza badala ya kuchokozana'' , alisema msemaji wa waziri wa maswala ya kigeni Lu Kang.Urusi pia ilitoa wito wa kuvumiliana .
Msemaji wa ikulu rais Dmitry Peskov alisema kuwa Moscow ina wasiwasi kuhusu kiwango cha wasiwasi kinachozidi kuongezeka.
Korea Kaskazini imekuwa ikifanyia majaribio makombora yake katika kiwango kisicho cha kawaida na kufanya jaribio lake la sita la kinyuklia licha ya shutuma za kimataifa.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Korea Kaskazini Ri Yong -ho ambaye awali alikuwa ameifananisha hotuba ya rais Trump kama ile ya ''mbwa anayebweka'' ameonya kuwa Pyongyang italifanyia jaribio bomu lake la H-Bomb katika bahari ya pacific kujibu tishio la rais Trump.
''Bomu hilo litakuwa bomu lenye uwezo mkubwa kuwahi kurushwa katika bahari hiyo ya pacific'' , Bwana Ri alisema akinukuliwa na shirika la habari nchini Korea Ksakzini Yonhap.
Hatahivyo, aliongezea: Hatujui ni hatua gani zitachukuliwa na rais Kim jong-un

China yaiwekea vikwazo Korea Kaskazini

China yaiwekea vikwazo Korea Kaskazini
Magari ya kubeba mafuta kotoka China Kueleka Korea Kaskazini
Uchina imeimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini, ambapo imetangaza usitishaji wa ununuzi wa nguo kutoka Korea kaskazini mbali na uuzaji wa mafuta kwa taifa hilo kuanzia leo na baada ya muda fulani.
Hatua hiyo inaambatana na maagizo ya vikwazo yaliyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku 11 zilizopita.
Wachanganuzi wanasema kuwa vikwazo hivyo vitaathiri sana raia wa Korea Kaskazini iwapo vitatekelezwa kwenye mpaka kati ya mataifa hayo ambao hauna doria ya kutosha.
Rais Kim Jong Un wa KOrea kaskazini amesema kuwa rais Trump atalipia kauli zake katika mutano wa umoja wa mataifaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais Kim Jong Un wa KOrea kaskazini amesema kuwa rais Trump atalipia kauli zake katika mutano wa umoja wa mataifa
Utengenezaji wa nguo ni huduma muhimu ya pili inayoletea Korea Kaskazini fedha za kigeni na sehemu nne kwa tano ya nguo hizo hupelekwa Uchina.
Inakisiwa kuwa zaidi ya watu 100,000 wanafanya kazi katika sekta hiyo nchini Korea Kaskazini.

Iran yafanyia majaribio kombora lake

Iran inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la Khorram-shahr.
Iran inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la Khorram-shahr.
Kombora hilo lilionyeshwa hadharani katika maonyesha ya kijeshi jana Ijumaa.
Iran imesema kuwa kombora hilo linaweza kusafiri mwendo wa kilomita 2,000.
Kituo cha runinga cha taifa hilo kilionyesha picha za sherehe hizo.
Kombora la kwanza la Khorram-Shahr lilirushwa angani Januari lakini likalipuka katikati ya mwendo.

Tetemeko la ardhi lasikika Korea Kaskazini, Je ni jaribio la kombora?

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 3.4 katika vipimo vya Ritcher limesikika nchini Korea Kaskazini.

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 3.4 katika vipimo 

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 3.4 katika vipimo vya Ritcher limesikika nchini Korea Kaskazini.
Tetemeko hilo lilitokea kilomita 50 kutoka kituo cha majaribio ya makombora ya kinyuklia .
Mitetemeko mengine ya ardhi imetokea wakati wa majaribio ya makombora.
Wataalam wa mitetemeko nchini China wamesema kuwa wanatuhumu ulikuwa mlipuko.
Lakini Korea Kusini inasema kuwa huenda ni tetemeko la kawaida ambalo halikusababishwa na jaribio la kombora la kinyuklia.
Korea Kaskazini ilifanya majaribio makubwa ya kombora lake la kinyuklia mnamo Septemba 3 ambalo limeshutumiwa pakubwa katika mkutano wa umoja wa mataifa.
Kiwango cha tetemeko la siku ya Jumamosi ni kidogo ikilinganishwa na wakati taifa la Korea Kaskazini linapofanyia majaribio makombora yake. Ritcher limesikika nchini Korea Kaskazini.

JUX -UTANIUA

UKARABATI WA MAJENGO CHUO CHA UWANDISHI WA HABARI ARUSHA


Baadhi ya wanafunzi katika chuo cha uwandishi wa habari na utangazaji Arusha wametoa maoni yao kuhusu ukarabati wa majengo unaofanyika chuoni hapo.

wanafunzi hao wametoa maoni yao mapema hii leo walipokuwa wakizungumza na KAPONDO HOT NEWS .

Bw Matthayo Kijazi ambae ni mmoja wa wanafunzi chuoni hapo amesema ukarabati huo umeungwa mkono kwani kuna faida kubwa kwa majengo hayo kuboreshwa.

nae Bi Suzan Kimaro amesemakuwa ujenzi wa majengo hayo yataweza yataweza kuwafanya wasome vizuri kuliko hapo mwanzo.

Na mkuu wa chuo hicho Bw Andrew Ngobole kuwa lengo la kuboresha majengo hayo ni kufanya wanafunzai waweze kusoma katika mzngira bora na rafiki.
Hata hivyo ujenzi wa majengo hayo utakamilika November mwaka huu.

Diamond Aamua Kumfuata Mama Watoto Wake 'Zari' Afrika Kusini

Diamond Aamua Kumfuata  Mama Watoto Wake 'Zari' Afrika Kusini Diamond Aamua Kumfuata  Mama Watoto Wake 'Zari' Afrika Kusini
Ikiwa zimepita siku nne tangu mwanamuziki Diamond Platnumz akiri kumsaliti mpenzi wake Zari, hatimaye ametua nyumbani kwa mwanamke huyo nchini Afrika Kusini.

 Leo saa 5.40 asubuhi mwanamuziki huyo aliposti video katika mtandao inayomuonyesha akicheza na mtoto wake wa kwanza, Latifah huku kwa mbali ikisikika sauti ya Zari.

Dada wa mwanamuziki huyo, Esmah Khan aliposti video hiyo katika mtandao wa Instagram: “Tuko na Tiffah na mamy tunaita raha ya mtoto apewe mapenzi kwa baba na mama jamani.”

Leo ilikuwa siku muhimu kwa Zari kwani anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Iran yafanyia majaribio kombora lake

Iran inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la Khorram-shahr.
Kombora hilo lilionyeshwa hadharani katika maonyesha ya kijeshi jana Ijumaa.
Iran imesema kuwa kombora hilo linaweza kusafiri mwendo wa kilomita 2,000.
Kituo cha runinga cha taifa hilo kilionyesha picha za sherehe hizo.
Kombora la kwanza la Khorram-Shahr lilirushwa angani Januari lakini likalipuka katikati ya mwendo.Jaribio hilo lilifanywa siku chache baada ya Rais Trump wa Marekani kushambulia Iran katika hotuba yake katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Rais wa Iran, Hassan Rouhani, ametetea hatua ya taifa lake kuimarisha zana zake kwa lengo la kujitetea.

Iran inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la Khorram-shahr.

Mbowe Atoa Sababu Kwa Nini Hawajafungua Kesi Yoyote Dhidi ya Shambulio la Tundu Lissu


Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe amefunguka na kujibu hoja za kwa nini mpaka sasa CHADEMA hawajafungua kesi kutokana na shambulio Tundu Lissu  ambapo amesema ni kutokana na kuwa kipaumbele chao cha kwanza ni kuokoa maisha ya Lissu.

Mh. Mbowe ameyasema hayo wakati akizungumza jana na wanahabari ambapo amesema kuwa baada ya tukio la Lissu kutokea akili na mawazo ya Chadema yalikuwa kwenye kuokoa maisha ya Lissu na wanasubiri mambo yakiwa sawa wataangalia kufanya lolote linalowezekana kwan wakati huo.

"Kwa nini Chadema hatujafungua kesi? Kesi unafungua kwa nani? Anayechunguza ni nani? Chadema tumeshafungua kesi nyingi ya akiwepo Ben Saanane msaidizi wangu aliye[potea kusikojulikana, Kesi ya nyani unapeleka kwa Tumbili. Priority yetu sisi ni kumuokoa Lissu na siyo Kesi. Kupigania maisha yake ndicho kitu tuliona kinachofaa kufanywa na ndicho tunachofanya mpaka sasa", amesema.

"Ninaamini tu mambo yakikaa sawa vichwa vyote hivi vya Chadema vitajua kama tunaweza kufungua kesi au kitu gani kingine ambacho kinafaa kufanywa endapo tu afya ya Mh. Lissu ikishaimarika" ameongeza

Akizungumzia kwanini mpaka leo dereva wa Lissu hajarudi nchini ili kwenda kuripoti polisi kama jinsi jeshi la polisi lilivyoagiza, Mbowe amesema kwamba kijana huyo atarudishwa nchini pindi tuu wataalamu wa afya wanaomhudumia wakitoa ripoti afya yake kama iko salama na wao hawapo kwa ajili ya kumficha.

"Wiki iliopita nilisema dereva wa Mh. Lissu yupo Nairiobi kwa ajili ya matibabu ya kisaikolojia. Hatukuona kama ni busara kumtelekeza wakati alikuwepo kwenye matatizo na boss wake. Madaktari wakituthibitishia kuwa yuko timamu atarudi nchini kwani hatuko kwa ajili ya kumficha mtu. Yule kijana ni kama mtoto wa Lissu, dereva na mlinzi wake, wana miaka mingi pamoja tangu Lissu anagombea ubunge kwa mara ya kwanza" amesisitiza.

Ameongeza pia dereva atakuja kuzungumza nini kilitokea na yeye alijiokoaje naamini aliyekuwa anashambulia alikuwa hajalenga kumuacha hai mtu hata mmoja hivyo mimi siyo msemaji sana wa dereva wake Lissu lakini akipona ataelezea mwenyewe kila kitu.

KAZI KAZI YA LIGI KUU BARA WIKIENDI HII, IKO HIVI...

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Septemba 23, mwaka huu kwa michezo mitatu kuchezwa katika viwanja tofauti hapa nchini.

Kesho Jumamosi Young Africans itacheza na Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa Mwadui ya Shinyanga katika mchezo utaofanyika Uwanja wa Mwadui.

Mchezo mwingine, utakutanisha timu za Majimaji itakayokuwa mwenyeji wa Njombe Mji kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Mechi zote hizo zitaanza saa 10.00 jioni.

Jumapili Septemba 24, mwaka huu kutakuwa na michezo minne ambako Ruvu Shooting itaialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani huku Stand United ikicheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga. Mechi hizo pia zitaanza saa 10.00 jioni.



Michezo mingine itakuwa ni Singida United itakayoialika Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma saa 10.00 jioni kabla ya Azam kuialika Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi katika mchezo utakaoanza saa 1.00 jioni